Wednesday, February 13, 2013

MAANA YA SIKU YA WAPENDANAO( Valentine Day)


Siku ya wapendanao ni sikukuu ambayo huadhimishwa kila ifikapo tarehe 14 Februari ya kila mwaka (Valentine Day).
Historia yake imeanzia karne ya 3 huko Roma ambapo alikuwapo padri Valentinus ambaye akaja kuheshimiwa kama mtakatifu hasa tarehe hiyo
Inasemekana kwamba Kaisari wakati huo alikuwa Claudius II: yeye aliona kuwa askari mkakamavu na bora zaidi ni yule asiyeoa wala kuwa na familia (kapera). Hivyo alipiga marufuku ndoa kwa askari.
Valentinus alipinga jambo hili hivyo kuendelea kufungisha ndoa kwa siri. Mfalme Claudius alipopata habari hizi aliamuru Valentinus akamatwe na kuuawa.
Kuna hadithi nyingine ya kuwa akiwa gerezani Valentinus aliandika barua ambayo ilikuwa na salamu za kwanza za Valentine kwa binti aliyeenda  kumsalimia gerezani; mwisho wa barua alihitimisha kwa maneno haya: Kutoka kwa Valentinus wako.
Toka hapo Valentine anakumbukwa kama mtetezi wa wapendanao na sikukuu yake kuadhimishwa kote duniani.




Monday, July 23, 2012


Diwani wa CCM afa ghafla, alianguka

DIWANI wa Kata ya Mianzini iliyopo Mbagala Charambe jijini Dar es Salaam, Cesylia Macha, amefariki dunia ghafla wakati alipokuwa akizungumza na wajumbe wa kata hiyo

Diwani huyo alianguka juzi katika ofisi za CCM eneo la Kibonde Maji akwia katika mazungumzo na wajumbe wa kamati ya siasa wa kata hiyo na alikimbizwa Zahanati ya Zakhiem kupatiwa matibabu na alifariki akiwa njiani kuelekea huko.


Imedaiwa diwani huyo alikuwa amesimama wakati alipokuwa akifanya mazungumzo hayo na kabla hajakaa kwenye kiti alianguka ghafla

Kifo hicho kimethibitishwa na Mwenyekiti wa kata hiyo Bw. Hakika na kusema walipomfikisha hospitalini hapo wakati wakiwa katika vipimo daktari alisema alishafariki dunia

Amesema maziko ya diwani huyo yanatarajiwa kufanyika leo saa 10 alasiri nyumbani kwake

Akitoa kwa kifupi historia ya marehemu alifafanua kuwa - Diwani huyo alijiunga na CCM mwaka 1977.

Mwaka 2000 aliamua kugombea ujumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Kata ya Charambe na ujumbe wa kamati ya siasa ya kata na kushinda nafasi zote hizo.

Mwaka 2005 aligombea udiwani wa Kata ya Charambe kupitia CCM na kuibuka mshindi

Mwaka 2010 aligombea udiwani kupitia CCM katika Kata ya Mianzini ambayo ilianzishwa baada ya kugawanywa kwa Kata ya Charambe ambako aliibuka kidedea.

Wednesday, January 26, 2011

LAMAR AFAGILIA KILL 2011


Produza mahiri wa Muziki hapa nchini Lamar anayemiliki studio ya Fishcrab, amesema ana imani kubwa na tuzo za Kill Music Awards za Mwaka huu tofauti na miaka mingine iliyopita.
Lamar amesema ataendelea kufanya kazi zake kwa ubora ule ule kama ilivyo kawaida yake na kwamba
hatokubali kuona anarudi nyuma katika utayarishaji wake wa Muziki kwa wasanii wote watakaohitaji kufanya kazi zao an yeye.
Lamar pia alisema tofauti na matarajio ya wengi kuhusu tuzo za Kill Music Awards, yeye binafsi ana amini kuwa tuzo hizo zimeandaliwa kwa ubora wa hali ya juu hivyo kupelekea yeye kuwa na imani nayo.
Alisema kimsingi Kampuni ya bia ya TBL kupitia bia yake ya Kilimanjaro wamefanya kitu kikubwa kwa kuwawezesha watanzania kuwachagua wanamuziki wenye uwezo hasa wanaowaona ili kuwawezesha kupata tuzo hizo.
Alisema anafurahishwa na ujio wa tuzo hizo kwa mwaka huu huku akiamini kuwa lengo lake ni kuwapata wanamuziki bora na siyo bora wanamuziki katika kukuza sanaa hiyo hapa nchini.

WASANII PIMENI UKIMWI MTAMBUE AFYA ZENU - BASATA

Kaimu Mwenyekiti Jukwaa la Sanaa ambaye pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Utafiti, Mafunzo na Habari, BASATA George Lebejo Mngereza akizungumzia swala la wasanii kupima ukimwi.

Mwandishi Wetu

Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limewataka wasanii na wadau wa sanaa kwa ujumla kujenga utaratibu wa kupima UKIMWI mara kwa mara ili kutambua afya zao na baadaye kuweza kupanga mipango yao ya maisha na shughuli zao za sanaa.

Rai hiyo imetolewa na Kaimu Mwenyekiti Jukwaa la Sanaa ambaye pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Utafiti, Mafunzo na Habari, BASATA George Lebejo Mngereza wakati wa zoezi maalum la kupima UKIMWI kwa hiari lililoendeshwa na program ya Jukwaa la Sanaa kwa kushirikiana na Shirika la AMREF kupitia mradi wa Angaza.

“Wasanii wamekuwa mstari wa mbele kuhamasisha watu wengine kupima UKIMWI huku wao wenyewe wakibaki nyuma wakati wako katika mazingira hatarishi ya kuambukizwa,nadhani sasa wanapaswa nao kuwa mstari wa mbele katika kutambua afya zao ili sasa waweze kupanga mikakati katika shughuli zao za sanaa na maisha yao kwa ujumla” alisema Mngereza.

Aliongeza kwamba BASATA imekuwa ikitoa fursa mbalimbali za mafunzo dhidi ya UKIMWI kwa wasanii ambayo yamekuwa yakiambatana na zoezi la upimaji kwa hiari na lengo kuu la zoezi hilo ni kuwapa fursa wasanii ambao wamekuwa wakitumiwa kama daraja la kuhamasisha watu mbalimbali nao kufahamu kwa kina gonjwa hili na kujua jinsi ya kuliepuka lakini pia kutambua afya zao ili kuishi kwa tahadhari.

“Sote tutakumbuka kwamba Oktoba 25 mwaka jana BASATA iliendesha zoezi kama hili la elimu dhidi ya UKIMWI kwa wasanii na upimaji. Hii ni fursa nyingine kwa wasanii na wadau wa sanaa kwa ujumla kufanya hivyo ili kutambua afya zao” alisisitiza Mngereza.

Katika zoezi hilo ,jumla ya wadau 187 walihudhuria kwenye Jukwaa la Sanaa ambapo kati yao 107 walipata fursa ya kupima kwa hiari na hakuna hata mmoja aliyekutwa ameathirika.Idadi hii ni ni zaidi ya wale wa zoezi lililopita kwani 79 tu ndiyo walipima.

Awali kabla ya zoezi la kupima, Mkurugenzi wa Kundi la Sanaa la Parapanda Mgunga Mwamnyenyelwa aliwasilisha mada kuhusu Jinsi ya Kuifanya Sanaa na Utamaduni Wetu kutambulika kimataifa ambapo alisisitiza umuhimu wa wasanii wa muziki kuzingatia fani na maudhui ili kuweza kuzifanya kazi zao kuvuka kimataifa.

Aidha,alitumia fursa hiyo kutangaza tamasha kubwa la tamthiliya linalotazamiwa kuanza Januari 28 na kumaliza Januari 29, 2011 kwenye Ukumbi wa Utamaduni wa Ubalozi wa Urusi ambapo litahusisha wanafunzi wa shule mbalimbali za sekondari na baadaye wadau wengine.

Thursday, December 2, 2010

PEPE KALEE MIAKA 12 SASA TANGU AFARIKI

Pepe Kalle Miaka 12 sasa Afrika bado yamlilia

Mbali na kuwa na utajiri wa madini ya kila aina, Bara la Afrika limejaaliwa kuwa na utitiri wa watu wenye vipaji katika nyanja mbalimbali katika ulimwengu huu.

Leo hii ukizungumzia mchezo wa soka basi ndani yake kutakuwa na mlolongo wa majina ya wasakata kabumbu, wanariadha, wanamuziki nakadhalika kutoka bara hili ambao wanatamba kote duniani.

Kwa namna moja ama nyingine hawa ni watu ambao tunaweza kuwaita mashujaa wa bara letu kwa kuweza kulitangaza vizuri kupitia fani zao mbalimbali.

Jumapili iliyopita Afrika ilikua inaadhimisha kumbukumbu ya miaka 12 tangu kifo cha nyota wa muziki wa Kwasakwasa wa DRC Kongo, marehemu Kabesele Yampanya ‘Pepe Kalle’

Akiwa na sauti za mirindimo mbalimbali na uwezo wa kubadili mbinu zake za uchezaji wa shoo, Pepe Kale alirekodi nyimbo zaidi ya 300 na albamu zaidi ya 20 katika kipindi cha miongo miwili ya uimbaji wake.

Akijulikana kama Tembo wa Muziki wa Afrika, Pepe Kalle aliwafurahisha mashabiki wake kwa kiwango cha hali ya juu katika uimbaji na pia ubunifu wa mitindo kadhaa iliyokuwa ikinogesha muziki wake.

Alianza kuimba akiwa na bendi moja iliyojulikana kama African Jazz. Bendi hiyo ilikuwa ikimilikiwa na mwalimu wake wa muziki, Grand Kalle. Baadaye alikuja kuwa mwimbaji mkubwa wa Bendi ya Lipua Lipua ambapo alikuwa akiimba sambamba na mwimbaji mwingine aliyejulikana kama Nyboma MwandidoMwaka 1972, akiwa na wanamuziki wengine, Dilu Dilumona na Papy Tex, waliiacha Lipua Lipua na kuunda bendi yao iliyojulikana kama Empire Bakuba. Bendi hiyo ilianza kwa kupiga muziki wake maeneo ya Jiji la Kinshasa.

Pepe Kalle akiwa na mwanamuziki mwingine Zaiko Langa Langa waliiwezesha bendi hiyo kuwa maarufu kwa vijana katika jiji la Kinshasa. Wakiwa na nyimbo kama Dadou alioutunga yeye mwenyewe na Sango ya Mawa uliotungwa na Papy Sango, bendi hiyo ilikuwa ikikamata nafasi za juu kabisa kwenye chati mbalimbali za muziki nchini Kongo. Pepe Kalle na Papy Sango pia ndiyo waliotunga staili ya kucheza iitwayo Kwasakwasa.

Katika maadhimisho yao ya miaka 10 mwaka 1982, bendi yao hiyo ilipigiwa kura kuwa bendi bora zaidi nchini Zaire (sasa DRC Kongo). Katika miaka ya 1980, Empire Bakuba iliendelea kufanya shoo katika maeneo mengi huku ikitoa si chini ya albamu nne kwa mwaka.

Mwaka 1986, Pepe Kale akishirikiana na Nyboma, alitoa albamu iitwayo Zouke Zouke ambayo ilikuwa ni moja ya albamu zilizouza vizuri kwa miaka mingi. Lakini ushirikiano wa mwaka 1988 na Nyboma katika albamu iliyoitwa Moyibi ndiyo uliompa heshima kubwa katika Bara la Afrika.

Mwaka 1990, Pepe Kalle alitoa albamu ijulikanyo kwa jina la Roger Milla. Albamu hiyo aliitoa kwa heshima ya mwanasoka wa Cameroon aliyetesa enzi hizo, Roger Milla.

Mwaka 1992, bendi yake ya Empire Bakuba ilipata pigo kubwa la kwanza baada ya kifo cha mcheza shoo, Emoro aliyekuwa mfupi aliyeuawa walipokuwa nchini Botswana walikokwenda kufanya shoo.

Pamoja na pigo hilo, umaarufu wa Pepe Kalle uliendelea kuongezeka katika miaka ya 1990 ambapo alitoa albamu kama Gigantafrique, ‘Larger than life’ na ‘Cocktail’ zilizopendwa na mashabiki wengi.

Pepe Kalle alizaliwa Novemba 30, 1951 Jina lake halisi ni Kabasele Yampanya, alikufa Novemba 28, 1998 kwa shinikizo la damu.

PIGA KURA KUCHAGUA BORA ZA 2010


Muda umewadia kwa wapenzi wa filamu kuweza kuthibitisha BORA ZA 2010.
PIGA KURA kuchagua wale Bora wa 2010 kupitia

Makundi ya Filamucentral bora za 2010.
Msanii chipukizi wa mwaka
Muigizaji bora wa kike
Muigizaji bora wa kiume
Mwandishi bora wa Mswaada
Mchekeshaji Bora
Filamu Yenye Kava bora
Mtayarishaji bora wa filamu
Kampuni bora ya utengenezaji filamu
Msambazaji Bora
Muongozaji Bora

TWANGA PEPETA KUKAMUA SIKU YA FAINALI ZA MASHINDANO YA MITUMBWI JIJINI MWANZA

Baadhi ya Washiriki wa mashindano Mitumbwi yanayoendelea kufanyika hivi sasa katika mikoa ya kanda ya Ziwa wakijiandaa kwa mbio hizo za majini.
kazi ikiendelea.

Bendi maarufu ya muziki wa Dansi ya African Stars (Twanga Pepeta) watatoa burudani ya aina yake katika fainali za mashindano ya mitumbwi ya Balimi jijini Mwanza Jumamosi, tarehe 4 Desemba.
Akizungumzia maandalizi ya Fainali hizo; Meneja wa Bia ya Balimi Fimbo Butallah alisema; Kimsingi maandalizi yote yamekamilika, na timu zote zitawasili jijini Mwanza kesho (Ijumaa) tayari kwa mpambano huu wa aina yake. Tutakuwa na timu tano toka kila kituo kilichoshiriki ngazi ya awali ikiwa ni pamoja na Kigoma, Kagera, Mara, Visiwa vya Ukerewe (UK) na wenyeji Mwanza.
Ili kunogesha zaidi burudani hizi, zitakazofanyika katika eneo la Mwaloni, bendi ya Twanga Pepeta itatoa burudani kwa mashabiki watakaohudhuria fainali hizi. Hivyo tunawaomba wakazi wote wa Mwanza na maeneo ya jirani kujitokeza kuja kupata burudani za mashindano haya ambayo kwa sasa ndiyo mashindano yenye mashabiki wengi zaidi katika kanda ya ziwa.

Mashindano yataanza saa 3 asubuhi hadi jioni

SOKO KUU LA UHINDINI MBEYA LAWAKA MOTO

Takriban miaka mitatu baada ya kuungua kwa soko lililokuwa maarufu sana la Mwanjelwa, wakazi wa jiji la Mbeya, jana usiku wamekumbwa na simanzi kwa mara nyingine baada ya soko kuu la Uhindini, lililoko katikati ya jiji hilo kuteketea kwa moto.

Ingawa hadi sasa haijaweza kufahamika hasa nini chanzo cha moto huo wala hasara iliyotokana na moto huo, kumekuwa na taarifa zilizozagaa ambazo zinaelezea kuwa, chanzo cha moto huo ni hitilafu za umeme, ambao katika siku na muda wa tukio, ulikuwa unawaka na kukatwa kwa style ya indicator za gari.

Tukio la kuungua kwa soko hili, limeshabihiana sana na lile la miaka mitatu iliyopita wakati soko la Mwanjelwa lilipoungua, kwani ilikuwa kipindi kama hili, na hali hii imezua hofu miongoni mwa wakazi wa jijini hapa.

Mungu epushia mbali mabalaa haya. napenda kuwapa pole wale wote ambao kwa namna moja ama nyingine wameathiriwa na tukio hilo, nikitaraji kuwa mamlaka husika zitafanya uchunguzi wa kina juu ya tukio hilo na kutupatia taarifa za kitaalamu, zitakazowezesha wananchi na wadau mbalimbali kuwa katika hali ya tahadhari ili majanga mengine ya namna hii yasiendelee kuukumba mji wa Mbeya na maeneo mengine ya nchi.

Thursday, September 30, 2010

JACKLINE WOLPER

Kiukweli kweli kabisa wala sitanii, nampenda sana huyu dada anapokuwa kazini. utakubaliana na mimi kuwa anafanya vizuri sana, just keep it up Jacky

DR. GHALIB BILAL ALIPOKUWA MKOANI MBEYA

Mgombea Mwenza wa Urasi wa Tanzania kupitia CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal, akimnadi mgombea ubunge wa jimbo la Ileje, Aliko Kibona, wakati alipofika katika jimbo hilo jana Sept 29 kufanya mkutano wa kampeni katika kujiandaa na uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani unaotarajiwa kufanyika Oktoba 31 nchini kote. (Picha na Muhidin Sufiani)
Mgombea Mwenza wa urais wa CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal na mkewe Zakia Bilal, wakiinua mikono kuwasalimia wananchi wa Kijiji cha Ilembo Wilaya ya Mbeya Vijijini, wakati walipowasili kijijini hapo juzi Sept 28 kufanya mkutano wa kampeni.
Wananchi wa Kijiji cha Ilembo Wilaya ya Mbeya Vijijini, wakicheza ngoma ya asili ya kabila la Wanyakyusa, wakati wa mapokezi ya mgombea Mwenza wa urais wa CCM, Dk Mohamed Gharib Bilal, alipofika katika Kijiji hicho juzi Sept 28 kufanya mkutano wa kampeni.
Wananchi wa Kijiji cha Ilembo Wilaya ya Mbeya Vijijini, wakimsikiliza Mgombea mwenza wa urais wa CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal, alipokuwa akiwahutubia kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika kijiji hicho juzi Sept 28.

MAPOKEZI YA WANAMUZIKI WA FEREE GOLA WALIPOTUA DAR JANA

. Mwimbaji na rapa mahiri wa mwanamuziki Ferre Gola kutoka Jamhuri ya Demokrasia ya Congo anayejulikana kama (Shikito) akipewa escot na Baunsa mara baada ya kuwasili usiku wa kuamkia leo uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu J.K,Nyerere.(Kwa Wahusika naomba nidhamu ya Baunsa huyu ambaye kwa bahati mbaya sikuweza kulibaini jina lake mapema,naomba ichunguzwe kwa makini awapo kazini) .! Mwimbaji na rapa wa Mwanamuziki Ferre Gola kutoka Jamhuri ya Demokrasia ya Congo anayejulikana kama (Shikitu) akihojiwa na wanahabari kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu J.K,Nyerere, hata hivyo Kiongozi wao mwanamuziki Ferre Gola anatarajiwa kuwasili leo mnamo saa 12 jioni na anatarajia kufanya onyesho kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee kesho Ijumaa akishirikiana na bendi ya Mashujaa inayoongozwa na Mwanamuziki Jado Field Force. Mmiliki wa bendi ya Mashujaa ajulikanae kwa jina la Mama Sakina,akiwaomba radhi baadhi ya waandishi wa habari usiku wa kuamkia leo katika uwanja wa kimataifa wa Mwl JK Nyerere,Kufuatia kutukanwa kwao na baadhi ya Mabaunsa waliofika uwanjani hapo huku wakiwa wamelewa,Mama Sakina pia alitoa ufafanuzi wa vurugu zilizotokea uwanjani hapo wakati wa kumpokea Ferre Gola,akieleza kuwa watu hao walikuwa wametumwa kwa ajili ya kuja kumuharibia mapokezi hayo wakiwemo na baadhi ya Mabaunsa ambao walikuwa wamelewa kupita kiasi huku wakitukana matusi mazito mazito kwa Waandishi wa habari waliokuja uwanjani hapo kufanya kazi yao. Mwanamuziki mpiga gitaa la Sollo kutoka kundi la Ferre Gola anayejulikana kama Chally Sollo akihojiwa na vyombo vya habari kwenye uwanja wa ndege wa Mwalimu J.K. Nyerere mara baada ya kuwasili kwa ajili ya onyesho lao linalotarajiwa kufanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee kesho Ijumaa. Baadhi ya Wanamuziki wa Bendi ya Mashujaa wakiongozwa na kiongozi wa bendi hiyo Jado Field Force (haonekani pichani) katika kutia nakshi nakshi ujio wa mwanamuziki Ferre Gola (Shetani) wakati walipokuwa wakimsubiri mwanamuziki huyo kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu J.K.Nrerere usiku wa kuamkia leo, pamoja na shamra shamra hizo Mwanamuziki huyo hakuweza kuwasili usiku wa jana,badala yale anatua leo jioni jijini Dar mnamo majira ya saa 12 na ushehe hivi,waliotangulia ni wanamuziki wake.

MIKE TEE KUITEKA MBEYA


Msanii anaeendelea kuiteka Tanzania kunako bongo fleva, MIKE TEE a.k.a mnyalu, amesema kwa sasa amehamia mbeya kwa shughuli zake, lakini kuhusu muziki bado anaendeleza makamuzi. Ndani ya mwaka huu mnyalu ametoa nyimbo mpya mbili, moja inaitwa I LOVE YOU na nyingine inaitwa TUJIIBE TUKIWEZA.

Jamaa yupo mbioni kufanya video na ataifanyia hapa hapa mbeya. Kubwa zaidi MIKE TEE yupo katika harakati za kuhamishia studio yake hapa mkoani mbeya. Studio inaitwa MY KEY RECORDS, PRODUCER NI YEYE MWENYEWE MIKE TEE.



Wednesday, September 29, 2010

MISS TANZANIA 2010 AKABIDHIWA BENDERA TAYARI KUELEKEA CHINA

Mshindi wa taji la ulimbwende nchini Tanzania kwa mwaka 2010(Miss Tanzania 2010),Genevieve Emmanuel, asubuhi ya leo hii(kwa saa za Tanzania) amekabidhiwa rasmi bendera ya Tanzania tayari kabisa kwenda kuiwakilisha nchi katika mashindano ya ulimbwende ya dunia(Miss World 2010) yanayotarajiwa kufanyika huko Sanya nchini China tarehe 30 Oktoba 2010.Anatarajiwa kuondoka nchini kesho.

Shughuli ya kumkabidhi bendera mrembo huyo ilifanyikia katika viwanja vya Tanzania Investment Centre(TIC) jijini Dar-es-salaam na kuhudhuriwa na watu mbalimbali akiwemo Mkurugenzi wa kituo hicho cha uwekezaji,Bw.Emmanuel Ole Naiko, Miss Tanzania 2009,Miriam Gerald, Mratibu wa Miss Tanzania,Hasheem Lundenga,wawakilishi wa wadhamini wa shindano la Miss Tanzania kutoka kampuni ya mawasiliano,Vodacom na wengineo.

Miss Tanzania 2010,Genevieve Emmanuel(kushoto) na Miss Tanzania 2009,Miriam Gerald.

Mashindano ya mwaka huu yanaadhimisha miaka 60 tangu kuanzishwa kwa mashindano hayo.Awali mashindano ya mwaka huu yalikuwa yafanyikie nchini Vietnam lakini nchi hiyo ilijiondoa katika uandaaji huo na hivyo China kupewa nafasi ya kuyaandaa

Wednesday, September 8, 2010

REST IN PEACE P. DIDDY


HABARI ZILIZOTUFIKIA MUDA HUU, ZINASEMA KWAMBA MKURUGENZI MSAIDIZI WA BENDI YA MUZIKI WA DANSI YA DIAMOND MUSICA, PERFECT KAGISA 'P DIDY' AMEFARIKI DUNIA.
INAELEZWA P DIDY AMEFARIKI GHAFLA BAADA YA KUANGUKA, BARABARA YA LUMUMBA, MNAZI MMOJA, JIJINI DAR ES SALAAM ALIPOKUWA KATIKA MIZUNGUKO YAKE.TUNAENDELEA KUFUATILIA TAARIFA HII KWA UKARIBU NA TUTAWALETEA KILA KINACHOJIRI.

Monday, August 30, 2010

RAIS KIKWETE AKIWA TUNDUMA MKOANI MBEYA

Rais Jakaya Kikwete akihutubia umati wa wakazi wa Tunduma jioni hii wakati akianza kampeni yake mkoa wa Mbeya.
Rais Jakaya Kikwete akihutubia jioni hii mjini Tunduma ambako kumetia fora sana kwa umati mkubwa wa watu katika vituo vidogo vya mikutano ya kampeni za Chama tawala CCM
Uwanja wa mkutano Tunduma ulikuwa hautoshi
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Profesa Mark Mwandosya akimfagilia njia JK ya kuhutubia wananchi wa Tunduma leo

MGOMBEA MWENZA WA URAIS,DR. BILAL AKIWA ZIARANI MKOANI MTWARA

Mgombea mwenza wa urais kwa tiketi ya CCM,Dk. Bilal akizungumza na wanachi wa Wilaya ya Nanyumbu baada ya kuingia mpakani mwa wilaya hiyo na Masasi leo
Kamanda wa Chipukizi wa Wilaya ya Masasi, Fatuma Rajab akimvisha skafu Mgombea Mwenza Dk. Mohamed Gharib Bilal alipokuwa akiingia mpakani mwa Wilaya ya Masasi akitokea Wilaya ya Newala leo mchana
Mgobea Mwenza wa urais, Dk. Mohamed Gharib Bilal akisalimiana na wananchi na viongozi wa Chama cha Mapinduzi wa Wilaya ya Masasi, baada ya kuingia mpakani mwa wilaya hiyo na Newala, leo
Baadhi ya makada wa Chama cha Mapinduzi wa Wilaya ya Newala Mkoa wa Mtwara, wakiwa katika magari kwenye msafara wa kumsindikiza Mgombea Mwenza wa nafsi ya urais, Dk Mohamed Gharib Bilal, alipokuwa akitoka Wilaya hiyo kuelekea Wilaya ya Masasi leo asubuhi
wananchi wa Kijiji cha Lukuledi Wilaya ya Masasi Mkoa wa Mtwara, waliojitokeza kumsikiliza mgombea Mwenza Dk. Mohamed Gharib Bilal, alipokuwa akiwahutubia na kuwanadi wagombea Ubunge wa Jimbo la Lulindi,Bwanausi Dismas na Mariam Kasembe wa Jimbo la Masasi leo
Wananchi wa Kijiji cha Mangaka Wilaya ya Nanyumbu Mkoa wa Mtwara Jimbo la Nanyumbu, wakimsikiliza mgombea mwenza Dk. Mohamed Gharib Bilal, alipokuwa akiwahutubia wananchi wa Kijiji hicho leo mchana.

WAREMBO WA MISS TANZANIA WALIPOTEMBELEA MAPANGO YA AMBONI -TANGA

Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Said Said Kalembo (katikati) akizungumza na warembo wa .Vodacom Miss Tanzania 2010 ofisini kwake jana jijini Tanga. Kushoto ni Mkurugenzi wa lino International Agency Waandaaji wa shindano hilo Hashim Lundenga na Kulia ni Katibu Mkuu wa Kamati ya Miss Tanzania Bosco Majaliwa 'Mshua'. Warembo wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Tanga...

Warembo wa Vodacom Miss Tanzania 2010 wakipiga picha na watoto waliotembelea mapango ya Amboni mjini Tanga jana ikiwa ni sehemu ya ziara yao ya kutembelea vivutio vya utalii Kanda ya Kaskazini na kuhamasisha utalii wa ndani nchini.

Warembo wakionekana miguu tu ndani ya Mapango ya Amboni
Warembo wakitembea ndani ya Mapango ya Ambani mjini Tanga jana kujionea Mapango hayo ya asili ya kale ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha Utalii wa ndani nchini.
Warembo wakipita ndani ya mapango hayo ya Amboni..
Huyu ni mwakilishi wa Jiji la Tanga aliamua kupozi katika sehemu ambayo wanaisema inafanana na kiti.

M-Net’s Big Brother All Stars day 42

It’s day 42 on M-Net’s Big Brother All Stars ---and Sheila is evicted from the Big Brother All Stars house in show featuring Zambia’s Salma Dodia. She now joins Hannington, Lerato, Tatiana and Yacob in the Barn.

Stay tuned to M-Net’s BIG BROTHER ALL STARS with 24/7 coverage on DStv channel 198 plus daily edited shows on M-Net and AfricaMagic. For more information on the series, log on to www.mnetafrica.com/bigbrother. Pictured here: Jen, Code, Paloma

Friday, July 23, 2010

Flora Martin anyakua taji la Miss Higher Learning 2010

Miss Vodacom Higher Learning 2010,Frola Martin akipunga mkono mara baada ya kutangazwa mshindi katika shindano hilo

Miss Vodacom Higher Learning 2010,Frola Martin akipunga mkono mara baada ya kutangazwa mshindi katika shindano hilo lililofanyika usiku huu katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam, pili kulia ni mshindi wa pili Pendo Sam na pili kushoto ni Rachel Filbert mshindi wa tatu,kulia ni mshindi wa nne, Judith Osima na kushoto ni mshindi wa tano,Rahma Swai.
Tano Bora
washiriki wote wakiwa wamejipanga kabla ya mchujo wa tano bora
warembo wakionyesha shoo yao
Mangwer akifanya vitu vyake katika kusherehesha shindanano hilo lililomalizika usiku huu katika viwanja vya Karimjee,jijini Dar.
Quick Raca na Suma Lee wakionyesha vitu vyao jukwaani.

Vodacom foundation kudhamini Fashion 4 Health Black and Gold Gala

Mbunifu wa Mitindo nchini Tanzania, Mustafa Hassanali (katikati) akizungumza katika mkutano wake na Waandishi wa Habari Dar es Salaam leo juu ya Onesho la Mavazi la FASHION FOR HEALTH lililodhaminiwa na Vodacom Foundation litakalo fanyika Julai 30 2010 Visiwani Zanzibar. Kushoto ni Meneja wa Mfuko wa Vodacom Yessaya Mwakifulefule.

=========================

• Vodacom Foundation leads the way
• Mustafa Hassanali to launch “karafuu” collection in Zanzibar
• Fashion For Health in aid of the Zanzibar Mental Hospital

VODACOM Tanzania, through Vodacom Foundation, will this year sponsor a charity fashion show (Fashion 4 Health black & gold gala night) by Mustafa Hassanali in aid of the Zanzibar Mental hospital in Zanzibar on July 30th.

The show is being in Zanzibar for the third year in a row and is organized by Explore Zanzibar.

“As Zanzibaris it’s our responsibility and duty to accord a decent life to those seemingly neglected by society”, said Maryam Olsen, Managing Director of Explore Zanzibar.

To support her calling, Vodacom Foundation and Mustafa Hassanali have joined forces to create a synergy that will benefit various people at the Zanzibar mental hospital.

“This year we want to renovate the male ward and build a sports’ facility. For years, patients have been staying in sub-standard wards. Patients will be able to stay and learn in a fitting environment”, stated Mustafa Hassanali, who together with Explore Zanzibar supports the work of the Mental Hospital of Zanzibar (Kidongo Chekundu).

Mustafa Hassanali, Tanzania’s most renowned fashion designer shall unveil his new creations on the 30th of July 2010 at Zanzibar Serena Inn in Stone Town, with models from Dar es Salaam.

Zanzibar’s renowned designer, Farouque Abdella shall curtain raise the event together with Mago Designs. The show shall also feature a performance by the Tanzanite Band.

Mustafa Hassanali’s “Karafuu” Collection is inspired by the Cloves of Zanzibar. The multipurpose use of this Majestical spice is embodied in the fluid silhouette embodied in this black and gold collection.

“As per my tradition, one of my dresses shall be auctioned to assist in fundraising for this hospital with which I have been involved with since 2008” noted Mustafa Hassanali.

The Fashion 4 Health with the Vodacom Foundation Black and Gold Gala, has been sponsored by The Vodacom Foundation, PSI (Population Service International) African Life Assurance, Zanzibar Serena Inn, Explore Zanzibar, 361 Degrees Events and Vayle Springs LTD

ABOUT VODACOM FOUNDATION

Established in July, 2006, Vodacom Foundation focuses on the company's corporate social investment efforts with the aim of improving the welfare of Tanzanians.

The Foundation looks at four key areas, namely, education, health, economic empowerment and social welfare which are in line with the country’s national development priorities.

Foundation has carried out almost 100 projects in all the regions of the country and more are in the books. These projects have reached and have had direct impact on the lives of thousands of Tanzanians from an array of backgrounds.

ABOUT MUSTAFA HASSANALI

Mustafa Hassanali, a creative entrepreneur believes in the ‘never say die’ attitude and uses his talent and creativity in making a better today and tomorrow for the fashion fraternity along various social causes very close to his heart. Mustafa is truly a fashionista personified!

Mustafa’s work has been highly appreciated at international levels. His showing at the Afric Collection in Douala, Cameroon, India International Fashion Week 20009, Naomi Campbell’s Fashion for Relief 2009, Arise Africa Fashion week 2009, Durban & Cape Town Fashion Weeks, Vukani Fashion Awards in Pretoria, Miss Ethiopia Beauty Pageant, Mediterranean Fashion Festival in Sicily, Italy; M’Net Face of Africa, Mozambique, Uganda & Kenya Fashion Weeks has brought him immense adulation.

ABOUT ZANZIBAR MENTAL HOSPITAL

The Mental Hospital of Zanzibar (Kidongo Chekundu), built in 1947 during the British colonial period has been in dire need of funding for a long time. The year 2009 saw 6 million TSH raised. This has been used to create a female ward and an occupational therapy room, so that the patients could be divided and allow them the respect that for so long they’ve been denied, but deserved. The money was also used to improve the gardens and improve the therapeutic environment of the hospital.

ABOUT EXPLORE ZANZIBAR

Explore Zanzibar an event, tour and promotions company at the forefront of any major events in Zanzibar and always keen to break new ground while earning millions for charity. Its managing director is the executive secretary of ZATI, (Zanzibar Association of Tourism Investors) with over 110 businesses enrolled as members.

Wednesday, May 12, 2010

WATOTO WAFANYA KWELI

WATOTO WAKIWA KWENYE BUSTANI ZA MBEYA FM RADIO MARA BAADA YA KIPINDI



HAWA WATOTO JINSI MNAVYOWAONA JUMAMOSI HII WALIKUWA KWENYE KIPINDI, SASA WALIJADILI KUHUSU USAFI WA JIJI LA MBEYA. KATIKA KUJADILI WALIKUWA WANABISHANA SANA WENGINE WALIKUWA WANASEMA JIJI NI SAFI WENGINE JIJI NI CHAFU. WAKAULIZWA KWANI NI KAZI YA NANI KUWEKA JIJI KATIKA HALI YA USAFI? WAKAJIBU WATU WOTE WANA WAJIBU WA KUWEKA JIJI SAFI. WAKAULIZWA WAO WANAFIKIRI NINI KIFANYIKE JIJI LIWE SAFI? WAKASEMA MKURUGENZI WA JIJI ANATAKIWA KUFUATILIA NA KUJUA HALI YA USAFI IKO VIPI. KWA BAHATI NZURI MKURUGENZI AKAYASIKIA HAYO ,NA SASA KUNA WATU WAMECHAGULIWA NA JIJI KUFUATILIA USAFI NYUMBA HADI NYUMBA, UKIKUTWA NA UCHAFU WOWOTE UNAKAMATWA NA KUTOA ELFU 50.
MKURUGENZI WA JIJI HAKUAMINI KAMA HAWA WATOTO WANGETOA MANENO MAZITO VILE, KILA MTU SASA ANAJITAIDI KUWEKA MAZINGIRA SAFI.

Monday, May 10, 2010

VINARA WA MWAKA 2010

Monday, April 12, 2010

HIVI NDIVYO USINGIZI UNAVYOTAFUTWA...


Jamani kwa wale wageni ambao wanatarajia kwenda songea na hawana sehemu ya kufikia, hakika hapa ndio tulizo lako, unaweza kupata usingizi mnono.