Friday, November 27, 2009
Thursday, November 26, 2009
TULIANZA KAMA TIMU

HAWA WAKAJIONDOA KWENYE TIMU

Huyu anaitwa Peter Mlangi a.k.a dj P, alikuwa dj wetu lakini akaona kukaa mbali na my wife wake ni noma akaamua kuondoka na kwenda DSM kwa my wife wake. Alikuwa na busara sana na ni muelewa sana ila jamaa ana hasira ukimuudhi tu yeye ana mkono mwepesi sana, kwa hiyo haoni noma kukupa chako, nakukumbuka sana my brother
Wednesday, November 25, 2009
Sunday, November 22, 2009
HIVI NDIVYO MBEYA FM ILIVYOFANIKISHA MICHUANO YA KAPUNGA CUP 21.NOVEMBER.2009

MBEYA FM imeweza kufanikisha michuano ya Kapunga Cup ambayo ilianza rasmi tarehe
28.10.2009. michuano hii ilishirikisha timu za kata 36 za jiji la mbeya, na ziliundwa kanda nane
ambazo zilicheza hatua ya kwanza ambazo ndizo zilizokuja kucheza hatua ya robo fainali hadi fainali.
Fainali zimefanyika jana 21.11.2009 katika uwanja wa Ruanda Nzovwe na ilishirikisha kanda E na C.Kama tunavyojua katika mashindano lazima mshindi apatikane,
Kanda E iliibuka kidedea kwa penati na kuweza kujinyakulia kitita cha shilingi laki 5 kombe pamoja na jezi seti moja,
Mshindi wa pili alijinyakulia kitita cha shilingi laki 3, kombe dogo na jezi seti moja,
Mshindi wa tatu aliibuka na kitita cha shilingi laki moja na jezi seti moja.mfungaji bora alijinyakulia kitita cha shilingi elfu hamsini na ngao ya mfungaji bora.
Dhumuni la michuano hii ni kuhakikisha vijana wanapata nafasi ya kubadilishana mawazo, kuwaepusha na matumizi ya dawa za kulevya na makundi yasiyokuwa na msingi ambayo mwisho wake ni uhalifu. vilevile kupitia michuano hiyo tumefanikiwa kupata wachezaji watatu watakaojiunga na timu ya Tanzania Prisons inayoshiriki ligi kuu katika kipindi cha dirisha dogo la usajili wa ligi kuu ya soka Tanzania.
Mstahiki Meya wa jiji la Mbeya ATHANAS KAPUNGA ameishukuru MBEYA FM RADIO kwa kuandaa na kudhamini michuano hiyo kwa mwaka 2009.

MICHEZO FURAHA........... MICHEZO AFYA.................... MICHEZO HUJENGA MAHUSIANO MEMA.