
KISURA WA TANZANIA 2009
Shindalo hili la Kisura wa Tanzania 2009 limedhaminiwa na Serengeti Breweries Limited ambapo visura 19 wapo kambini kwa sasa.
Kuwa mwanamitindo si kujua kupanda jukwaani na kufanya catwalk tu bali uwanamitindo ni pamoja na kujua mambo mengi kama kujiamini, kutambua wewe ni nani, unaweza kuwa nani, kutambua kuwa unaweza kuleta mabadiliko katika jamii na nchi yako kwa ujumla, unaweza kushika hatamu ya maisha yako na kutambua ni uamuzi wako kutokupata ukimwi.
Hivi karibuni washiriki wa Kisura wa Tanzania 2009 walipewa jaribio kubwa sana la kupiga picha na nyoka uku wakiwa wamevalia nguo nadhifu za mbunifu maarufu hapa nchini, Fatuma Amor.
Zoezi ili lilikuwa ni gumu sana kwa visura wengi lakini kwa ajili ya uelewa wao, kujiamini kwao na ujasiri wao waliweza kupiga picha kama wanamitindo wa kimataifa wakiwa na bonge la chatu.
Shindalo hili la Kisura wa Tanzania 2009 limedhaminiwa na Serengeti Breweries Limited ambapo visura 19 wapo kambini kwa sasa.
Siku ya Jumapili, Novemba 29 Visura wote waliwekwa kwenye Ukanda wa hatari ili kuwapa fursa ya watazamaji wa TBC1 na watanzania wote kwa ujumla kupata nafasi ya kuchagua visura 10 tu ambao wanatakiwa kuingia kwenya fainali.
Kumpigia kura mshiriki unayempenda aingie kwenye top 10 andika neno Kisura acha nafasi halafu andika namba ya mshiriki kama zinavyoonekana mbele ya jina la kila mmoja wao, halafu tuma kwenda namba 15771.
Mshindi wa Kisura wa Tanzania 2009 anategemewa kutangazwa tarehe 18 Decemba pale kwenye hoteli ya kitalii Movenpick.
Wadhamini wengine wa shindano la Kisura wa Tanzania 2009 ni Kiromo View Hotel, Family Health International (FHI), TBC1, Air Tanzania, Mwananchi Communication, Clouds FM, Hugo Doming, Mercy G Beauty Parlour na EM Entertainment
Beautiful Tanzanie Agency (BTA)
1 comment:
Ooooohhh HELL NOOO
Hujanibebesha hilo lidubwashika hata kama ni "toy"
Nisivyoyapenda. Hivi walilala hao usiku?
Duh!!!!!!!!!!!!!
Post a Comment