Kampuni ya Bia ya Serengeti katika kusheherekea siku ya wapendanao (Valentine Day) inayoadhimishwa kila tarehe 14 Februari duniani kote, Imeandaa maeneo maalumu nane katika mikoa sita kwa ajili hiyo. Wanamuziki maarufu pamoja na mziki wa nguvu utakuwepo kuwaburudisha wananchi sambamba na bia yao ya Premium Serengeti Lager.
Dar es Salaam pekee, kutakuwa na sehemu muafaka tatu kwa ajili hiyo.
Club Bilicanas iliyopo katikati ya jiji la Dar es Salaam itakuwa nawe pamoja na Premium Serengeti Lager, wasanii maarufu wa Bongo Flava watakuwepo pamoja na disco lilokwenda shule.
Onesho lingine lililoandaliwa na Manywele Entertainment na kudhaminiwa nasi litakuwa pale katika Hoteli ya Travertine, kama kawaida kundi linalotisha na kuongoza afrika mashariki Jahazi Modern Taarab litakonga nyoyo za mashabiki huku wakisindikizwa na mwanamuziki Nyota Ndogo kutoka Kenya.
Klabu ya Rainbow Social iliyopo katika maeneo tulivu ya Mbezi Beach haitakuwa nyuma kusherekea Valentine pamoja na Premium Serengeti Lager.
Ndani ya Klabu hiyo itakuwepo Bendi ya Karunde, moja ya bendi zinazovuma sana jijini Dar es Salaam na nchini kwa ujumla.
Mbali na Dar es Salaam, Premium Serengeti Lager imeandaa shoo kamambe kwa wakazi wa Arusha katika klabu ya Via-via, Moshi pale katika Hoteli ya Salsalinero, Musoma Premium Serengeti Lager itasherehekea nawe pale Matvilla Hotel. Wakazi wa Mbeya watajivinjari pale Paradise Hoteli, huku wakazi wa Mwanza wakiwa na Chui-chui pale Lavena Beach Resort. Maonesho yote yataanza saa 3 za usiku.
Mbali na burudani hizo kutakuwa na zawadi kwa washindi. Vigezo vitakavyotumika kuwapata washindi, ni vazi rasmi lenye rangi nyekundu ama mchanganyiko wa nyekundu na nyeupe. Unaweza kuwa mshindi ukiwa umevaa rangi ya Chui-chui. Washindi watapata zawadi murua, zikiwepo t-shirt za hadhi ya juu, kofia na bia (take away) kwa kila mshindi.
No comments:
Post a Comment