Mkurugenzi wa Mikutano na Masoko wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC), Bi. Mkunde Senyagwa (kushoto) akikabidhi msaada wa vyakula na vifaa vya shule kwa Mwenyekiti wa Kituo cha Kulelea Watoto yatima cha Tumaini Positive, Bw. Emmanuel Ndolimana (kulia) ikiwa ni sehemu ya mpango wa AICC wa uwajibikaji kwa jamii. Makabidhiano hayo yalifanyika jana katika ofisi za kituo hicho cha yatima eneo la Kwangulelo, nje kidogo ya Mji wa Arusha. Waliosimama nyuma ni watoto wa kituo hicho na wafanyakazi wa AICC. (Picha kwa hisani ya AICC)
Wafanyakazi wa AICC, Emmanuel Mbise na Rodney Thadeus wakishusha msaada wa vyakula na vifaa vya shule kwaajili ya kituo cha watoto yatima cha Tumaini Positive. AICC ilikabidhi msaada huo ikiwas ni sehemu ya mpango wa AICC wa uwajibikaji kwa jamii.
Baadhi ya wafanyakazi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) kutoka kushoto ni Afisa Uhusiano Mwandamizi, Catherine Kilinda na Mkurugenzi wa Mikutano na Masoko, Mkunde Senyagwa wakiwa katika picha ya pamoja na walezi wa kituo cha kulelea yatima cha Tumaini Positive na watoto mara baada ya AICC kukabidhi msaada wa vyakula na vifaa vya shule kwa kituo hicho. Kulia kabisa aliyesimama ni Afisa Uhusiano wa AICC, Rodney Thadeus.
Watoto yatima wa kituo cha Tumaini Positive wakifurahia msaada wa vyakula na vifaa vya shule vilivyotolewa na Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) kwa kituo hicho jana. Msaada huo ni sehemu ya mpango wa AICC wa uwajibikaji kwa jamii.(Picha kwa Hisani ya AICC).
No comments:
Post a Comment