Thursday, December 31, 2009

HERI YA MWAKA MPYA KWENU WADAU


Habari Ndugu watembejeaji wa Blog hii,


Kwanza kabisa napenda kutoa shukrani zangu za dhati kabisa kwa Baba muumba wa Mbingu na Ardhi kwani yeye ndie muweza wa kila jambo.


Ndugu Wadau,tukiwa tunaelekea kuuaga mwaka 2009 na kuukaribisha mwaka 2010 napenda kuwashukuru sana tena sana kwa michango yenu mingi pia bila kuwasahau wale wote walioniwezesha mimi pamoja na Blogu yetu hii kufikia hapa,Nawashukuruni sana kwa woote maana mchango wenu,mawazo yenu ndiyo yaliyofanya kazi kubwa sana katika Blogu yetu hii.


Lakini pia naomba nitoe shukrani za pekee kwa watu wafuatao,nikianza na Othman Michuzi (Mzee Wa Mtaa Kwa Mtaa,Unaweza mtembelea kwa kupitia Hapa) ambaye ndiye aliyeniwezesha mimi kwa mawazo pia maoni ambayo yamenipa mwanga na kunifungulia njia, namshukururu sana Othman Michuzi kwa mchango wake mkubwa sana katika blog yangu,


Pili namshukuru sana Kaka Mubelwa Bandio (Mzee Wa Changamoto,Nae Mtembelee kwa hapa uone mambo yake) kwa changamoto zake juu ya blog,pia namshukuru kaka Agape Msumari (Mzee wa Viva Afrika,Gonga Hapa uone makeke yake)kwa mchango wake mkubwa,bila kumsahau kaka Ahmad Michuzi (Mzee wa Jiachie,nae anapatikana hapa) kwa mapendekezo yake juu ya blog yangu,


Lakini pia namshukuru Heriel Kachenje kwa ushauri wake na mwisho namshukuru Mkuu Enock Bwigane kwa maoni yake.na imani mwaka 2010 tutaendelea kuwa pamoja katika kuiendeleza blog yetu hii zaidi na zaidi.bila kusahau kumuombea Mzee wetu aliepoteza maisha siku ya leo,Mzee Rashid Mfaume Kawawa ili Mungu aweze kuiweka mahali pema peponi roho yake.


-Amin


nawapenda wote na nawatakia wote heri ya mwaka mpya 2010.


Wenu Katika Kuendeleza Blogu

Jaclnine Charles

1 comment:

Mzee wa Changamoto said...

How did i miss this?
Even though am late, i wanna say that I do Love and pray for you and your family every single night.
Thanx for the credit and i'm sorry for being out of touch for a while.
By the way
This is one of the best pictures of you. Loove it.
Stay Blessed and Safe

Post a Comment