Wednesday, March 10, 2010

MKESHA WA V.I.P MBEYA

Jahazi Modern Taarab ni bendi ya muziki wa taarab kutoka nchini Tanzania. Bendi ilianzishwa mwishoni mwa mwaka wa 2006, jijini Dar es Salaam. Jahazi Modern Taarab, ndiyo kundi linaloongoza kwa sasa katika miondoko ya taarab kwa nchi ya Tanzania, na ndiyo kundi pekee lenye washabiki wengi kuliko.

Kundi limeweza kujipatia mafanikio makubwa kabisa katika medani ya muziki wa taarab. Mzee Yusuf, ndiyo kiongozi na mmiliki wa kundi, ambaye pia ndiyo mwanamuziki mgunduzi wa mtindo wa taarab za kisasa (yaani “modern taarab”).

Mkesha wa pasaka yani tarehe 3.4.2010 Jahazi morden taarabu watakuwa wakiwatumbuiza wakazi wa jiji la mbeya, mkesha huo utajulikana kama MKESHA WA V.I.P, mkesha huo umeandaliwa na JAMA INTERTAINMENT ambayo iko chini ya Jackline Charles.

Mkesha huo unatarajiwa kuwa wa aina yake kwa sababu mara ya mwisho jahazi walifika mbeya mwaka 2007. mwanamama Isha Ramadhan nae atapewa fursa ya kuitambulisha album yake inayokwenda kwa jina la MAMA NIPE RADHI. Lakini pia tutakuwa tukigawana ustaarabu,

Show hiyo itafanyika ndani ya ukumbi wa mkapa kuanzia saa tatu usiku hadi saa tisa usiku.


2 comments:

viva afrika said...

safi sana hiyo, kamua dada yangu, mi huzimia sana mabinti wachapa kazi, kaza buti umlete hadi beyonce,,,,,,, pamojah sana.

Anonymous said...

jack acha uvivu tupe mambo kutoka mbeya hivi karibuni alitanguzwa mshindi wa maisha plus ni mkulima kutoka mbeye, nilivyoiona tu in other blog nikasema njoja nifungue blogs ya mrembo kutoka mbeya miss jack samahani kukuita miss pengine ni mrs,but nikaona kapa,mrembo chakarika napenda sana nipate habari kutoka mbeye si vyema kututupia habari moja kwa siku,sikufichi tangu niifumanie blog yako kupitia blog ya mtaa kwa mtaa hakuna siku ambayo sijapitia blog yako

Post a Comment