
Fid Q a.k.a Ngosha...Swaga Don akitoa burudani ya kutosha kwa wakazi wa Mbeya.

Mr Blue akitoa burudani kwa wakazi waliohudhuria tamasha la Shangwe na TIGO lilifanyika katika uwanja wa Sokoine Mbeya.

Baby Madaha a.k.a Baby Swaga akiwaonesha wakazi wa mbeye kipaji alichonacho cha kusheki bodi vilivyo kwa washabiki na wapenzi wamuziki wa kizazi kipya,kwenye tamasha la Shangwe na TIGO

Adamu Mchomvu ambaye alikuwa Mc wa shughuli hiyo akitambulisha wasanii waliokuwa wakitakiwa kutoa Burudani katika tamasha la Shangwe na TIGO.Tamasha hili liliratibiwa na kampuni ya Prime Time Promotions na Clouds Fm na kudhaminiwa na kampuni ya simu za mikononi ya Tigo pamoja na kampuni ya bia ya Serengeti.

Dully Sykes akiwaburudisha wakazi wa Mbeya na wimbo wake wa Shikide katika shwangwe na TIGO iliyofanyika mwishoni mwa wikend iliyopita katika uwanja wa Sokoine Mbeya.

Msanii wa bongofleva kutoka kundi la Wanaume TMK family,Chege Chigunda a.k.a mtoto wa mama Said akiwarusha vilivyo wakazi wa jiji la Mbeya kwenye tamasha la Shangwe na Tigo lililofanyika mwishoni mwa wikend.

Umati wa wakazi wa Mbeya wakishangilia kwa shangwe katika tamasha la Shangwe na TIGO lililofanyika katika uwanja wa Sokoine Mbeya wikend iliyopita.picha na
Jiachie Blog
No comments:
Post a Comment