Anaitwa Ayubu Byemelwa a.k.a Babu Ayubu mpaka sasa amefanikiwa kuikamilisha albamu yake ya kwanza ya taarabu ijulikanayo kwa jina la KOMBATI yenye jumla ya nyimbo nne, anazitaja nyimbo hizo kuwa ni Chaja ya kobe, Wapambe, Sendoff party pamoja na Jipu la kwapa, ambazo zote zimerekodiwa ndani ya studio za Sound Crafters Productions na Bakunde Productions.
Akifafanua mandhari nzima ya muziki wa taarabu kwa sasa, Babu Ayubu anabainisha kuwa umekuwa na tofauti kubwa, kwani muziki wa taarabu una asili yake na mashairi yake, asilimia kubwa ni mafumbo ambayo huimbwa kwa kumsema mtu au kumjibu mtu,

“Lakini zama hizi dhana nzima ya muziki huu imebadilishwa na baadhi ya wanamuziki kuufanya ni ulingo wa matusi, jambo ambalo linapelekea muziki huo kupoteza maana halisi ya taarabu” analonga Babu Ayubu.
Ambaye kwa sasa anatamba na wimbo wake wa Chaja ya kobe,yuko pale chuo kikuu huria akichukua shahada yake kwanza ya sociology .Picha na habari kutoka Jiachie Blog
No comments:
Post a Comment